MWIGIZAJI ALIYEFANYA UPASUAJI WA KUBADILI MWONEKANO AGEUKA KERO BOLLYWOOD

MWIGIZAJI mahiri wa filamu kutoka Bollywood, Ayesha Takia mwenye miaka 30, amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii akipingwa hata na mashabiki wake.

Msanii huyo aliyepata kuwa Miss India amefanya upasuaji wa kujibadili mwonekano, jambo ambalo limewaudhi watu wengi wakiwemo mashabiki wake ambao wanaamini amemkosoa Mwenyezi Mungu aliyemuumba.

Watu wengi wamemponda wakisema sura aliyojipa badala ya kumpendezesha, imemfanya aonekane kituko mbele ya watu, tofauti na ile aliyoumbwa nayo.

“Kwa hakika naona kama vile Ayesha Takia amejiharibu sura yake nzuri kwa upasuaji alioufanya,” alisema mmoja wa mashabiki wake.


Mbali na Ayesha Takia, wasanii wengine wa Bollywood waliowahi kujibadili muonekano wao na kupata upinzani kutoka kwa mashabiki na watu wengine ni pamoja na Anushka Sharma na Priyanka Chopra.

No comments