MWIGIZAJI NATALIE PORTMAN WA HOLLYWOOD APATA MTOTO WA KIKE

MWIGIZAJI mahiri wa Hollywood, Natalie Portman amebahatika kujifungua salama mtoto wa kike.

Msanii huyo aliandika katika mtandao wake wa kijamii akiwaarifu mashabiki wake kuwa bado hajampatia jina mwanae huyo.

Alisema anafurahi kuona mwanae ana afya nzuri na yeye mwenyewe yuko katika hali njema na kwamba madaktari wanaendelea kuwachunguza ili kujiridhisha iwapo hakuna madhara kabla ya kuruhusiwa.

No comments