Habari

NAPE AISHANGAA TFF KUKAA KIMYA PROGRAMU YA MICHEZO YA OLIMPIKI 2020

on

WAZIRI wa
Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amewashangaa viongozi wa
Shirikisho la soka Tanzania (TFF), kwa kukaa kimya kuhusu programu ya michezo
ya Olimpiki mwaka 2020.
Nape aliyasema
hayo wakati wa wadau wa michezo nchini uliofanyika wiki iliyopita, kuzungumzia
pamoja na mambo mengine, mikakati ya kimichezo kwa mwaka 2017.
Alisema,
inashangaza kuona TFF bado ipo kimya licha ya kufahamu kuwa inapaswa kufanya
maandalizi ya timu mbili za soka ya vijana chini ya miaka 23 na ile ya
wanawake.
“Nawashangaa
sana TFF kwa kuendelea kuwa kimya hadi sasa kuhusu program yao ya michuano ya
Olimpiki 2020, nia yetu kwa sasa ni kushiriki na kurudi na ubingwa, hatutaki
kwenda kutalii,” alisema Nape.

Alisema kuwa
ikiwa chama au shirikisho litawasilisha program mapema, serikali nayo itapata
muda wa kujipanga katika kuwasaidia kuhakikisha yanafanyika maandalizi ya
kutosha.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *