NEW AUDIO: “MWANAMKE MPANGO MZIMA” YA ISHA MASHAUZI …mseto wa chakacha, dansi na taarab
“Mwanamke Mpango Mzima” ni nyimbo mpya kabisa kutoka kwa Isha Mashauzi ikiwa ni mwendelezo wa ile project yake ya nyimbo fupi fupi nje ya bendi yake ya Mashauzi Classic.

Wimbo huu wenye ujumbe wenye ‘akili’ umegongwa katika miondoko ya chakacha na kukolezwa na vionjo vya dansi na taarab na kupelekea kuzaliwa kwa bonge la songi.

“Mwanamke Mpango Mzima” ambayo ina urefu wa dakika 3 na sekunde 55 imepakuliwa katika studio za Soft Records chini ya producer Pitshou Mechant.

No comments