NEW AUDIO: “SIJALI” YA MKONGWE WA RUMBA DELPHEE MUNUNGA
Baada ya kimya kirefu mwimbaji mkali wa muziki wa dansi Delphin “Delphee” Mununga aliyetamba na bendi kadhaaa zikiwemo Zaita Musica na Kilimanjaro Connection, ameibuka kigongo kikali cha rumba.

Delphee akiwa na project  mpya chini ya kundi lake litakalojulikana kama Viva Classic Band, ameachia kigongo hicho kilichopewa jina la “Sijali” kazi iliyofanywa chini ya producer Erasto Mashine.

Isikilize hapo juu ngoma hiyo mpya ya Delphee akisindikizwa na mdada mmoja matata mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni.

No comments