NEYMAR ASEMA BARCA HAIIFIKIRII REAL MADRID KUHUSU MBIO ZA UBINGWA

NYOTA wa Barcelona, Neymar amesema kuwa mabingwa hao watetezi wa La Liga hawawafikirii mahasimu wao Real Madrid katika mbio za kuwania ubingwa bali wanachofikiria wao ni kuongeza presha.

Katika mchezo wa juzi aliyeibuka tena kuwa shujaa alikuwa ni straika Lionel Messi ambaye aliifungia Barca bao la ushindi zikiwa zimebaki dakika nne kabla ya mchezo huo kumalizika na kuwafanya waondoke na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Atletico Madrid.

Kabla ya kupachika bao hilo matokeo yalikuwa ni 1-1 baada ya Diego Godin kusawazisha bao lililofungwa na Rafinha dakika ya 64 ya mchezo huo uliopigwa katika mji mkuu wa nchi hiyo.

Ushindi huo ni wan ne kwa Barca bila kufungwa na uliwahakikishia kuwa nyuma kwa pointi moja dhidi ya Real Madrid ambao bado wana mechi moja kibindoni baada ya kuwashinda Villareal kwa mabao 3-2.

“Hatuwazii timu nyingine, tunachotakiwa ni kujiangalia wenyewebinafsi,” alisema Neymar mara baada ya mechi hiyo.


“Wapinzani wetu wanaweza wakapambana ama wakashindwa. Nina furaha tumeshinda kutokana na kwamba tulikuwa tukifahamu mechi itakuwa ni ngumu na ninaipongeza timu nzima,” aliongeza nyota huyo.

No comments