NJOMBE MJI FC YAAHIDI KUFANYA MAKUBWA... yasema itahakikisha inashiriki na kushinda

TIMU iliyofanikiwa kupanda Ligi Kuu msimu huu ya Njombe Mji, imeweka hadhrani mikakati yake ikisema itafanya makubwa.

Akizungumza na saluti5, msemaji wa timu hiyo, Soranus Mhagama, alisema timu hiyo imejipanga kila idara.

Alisema kuwa benchi lao la ufundi  liko vizuri lakini pia uongozi hadi washabiki wamejipanga vizuri kuhakikisha watashiriki na kushindana.

“Sisi Njombe Mji tumejipanga vizuri na kuanzia sasa benchi la ufundi linaanza kuimarisha maeneo yote, hatutaki kushiriki na kushuka tunataka tushindane na tuwe washindani wa kweli,” alisema mhagama.


Timu hiyo iliungana na Singida United ya Singida na Lipuli ya Iringa, zilizolejea ligi kuu baada ya kusota madaraja ya chini kwa kipindi kirefu.

No comments