ORIGINAL DAR MUSICA YA JADO FFU KUPAKUA TATU MPYA WIKI IJAYO

WIKI ijayo Original dar Musica wanatarajiwa kutinga Studio za Amoroso Sound kupakua vibao vitatu vipya, imefahamika.

Akiongea na Saluti5, rais wa Original Dar Musica, Jado FFU amevitaja vibao hivyo ambavyo vyote ni makucha yake yeye mwenyewe, kuwa ni “Hatufanani”, “Jibebishe” na “Mtu Box”.


“Mashabiki wa Original Dar Musica wakae mkao wa kusubiri kwa hamu ujio wangu huu mpya ambao utamwagika mtaani baada ya wiki mbili na naamini utakuwa ni funika bovu,” amesema Jado FFU.

No comments