PEDRO ATIA MSISITIZO WA KUENDELEA KUBAKI NA KIKOSI CHA “THE BLUES”

STRAIKA wa matajiri wa Stanford Bridge, Pedro amesisitiza azma yake ya kuendelea kubaki Chelsea, licha ya kuweko na taarifa kuwa anajipanga kurejea Hispania.

Pedro alijiunga na “The Blues” akitokea Barcelona kwa dau la pauni mil 21.4lakini taarifa za sasa zinasema hana mpango wa kuondoka katika Ligi ya premier.

Klabu ya Atletico Madrid imekuwa ikitajwa katika orodha ya timu zinazomwania straika huyo mwenye umri wa miaka 28.

Akinukuliwa Pedro amesema: “Nina miezi minne kabla ya kumaliza mkataba wangu, lakini hilo halinipi presha kwa sababu ninaamini nitasalia hapa.”

“Nina furaha nikiwa hapa. Nayazungumza haya kwa imani ya moyoni. Ninajivunia kuwa katika klabu kubwa.”

“Nina furaha na mashabiki wa timu hii. Ingawa ni kweli kuwa hali ya mambo hapa si shwari hata kidogo, lakini kwa pamoja tunaweza kuipandisha timu kutoka hapa.”

“Ninaamini kwa kocha Antonio Conte. Ni kati ya makocha wazuri na klabu ina matarajio makubwa kwake.”


“Tayari ameonyesha imani kubwa kwangu, nami nina imani kubwa kwake. Ninaamini chini ya Conte timu ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu,” alisisitiza Pedro.

No comments