PEP GUARDIOLA AGOMA YAYA TOURE KUUZWA

KUNA taarifa kuwa klabu ya Paris Saint-Germain inahaha kwa hali na mali kutaka kumnasa kiungo mkongwe wa kikosi cha Manchester City, Yaya Toure.

Lakini taarifa za ndani ya matajiri hao zimesema kuwa, kocha wa sasa Pep Guardiola ameweka bayana kuwa kiungo huyo raia wa Ivory Coast hatouzwa kwa sasa.

Kauli ya Guardiola inakuja siku chache baada ya kocha huyo kuendelea kushutumiwa kwa kutowapa kipaumbele wanandinga wazoefu aliowakuta kikosini.

Tangu Pep Guardiola atue kwa ajili ya kukinoa kikosi cha matajiri wa jiji la Manchester, amekuwa akiwanyima namba katika kikosi cha kwanza wachezaji nguli waliokuwa imara katika kipindi ambacho timu ilikuwa ikifundishwa na Manuel Pellegrini.

Kati ya wachezaji hao ni pamoja na Yaya Toure ambapo pia amesababisha kuondoka kwa mlinda mlango, Joe Hart na kiungo Geofrey Bonny.

Akinukuliwa, Guardiola amesema Yaya ni mchezaji muhimu ndani ya kikosi na kwamba hatua ya kutakiwa na PSG ni kama uchokozi mkubwa.

“Kuna wanaoweza wakadhani kuwa Yaya sio kipaumbele change katika kipindi hiki cha ujio wangu hapa, hii sio sahihi kwasababu kila mchezaji ana nafasi ana umuhimu kulingana na mchezaji husika,” amenukuliwa Guardiola akizungumza na Sky Sports na kuongeza.

“Yaya Toure ni mchezaji muhimu katika kikosi cha City,” alisisitiza kocha huyo. “Lakini kunahitajika dau la kinajimu kuweza kuhonga na kwenda kokote.”

“Hatuiuzi klabu. Hatuna haja ya kuiuza. Tumejifunga kwa mchezaji wetu nae amejifunga kwetu.”

Muivory Coast huyo aliingia kwenye mzozo na kocha wake huyo kiasi cha kutokuwa na namba katika kikosi cha kwanza tangu Ligi premier ilipoanza, lakini amepangwa katika mechi za hivi karibuni na kuonyesha kiwango cha juu.


Aliingia katika mzozo na kocha wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich hadi ilifikia hatua ya Yaya Toure kuondoka akishirikisha azma na wakala wake.

No comments