PICHA 10: HIVI NDIVYO MASHABIKI WA TAARAB BUGURUNI WALIVYOLICHEZA JAHAZI NA MVUA LEKAM ROYAL HOTELUKWELI wa kwamba Jahazi Modern Taarab bado iko kwenye ubora wake ulijipambanua Jumamosi pale mashabiki walipojitosa kulicheza huku mvua kubwa ikiunguruma, ndani ya Lekam Royal Hotel, Buguruni, jijini Dar es Salaam.

Katika shoo hiyo iliyohudhuriwa na wapenzi wengi, Jahazi Modern iliyo chini ya Prince Amigo ilionekana kumimina burudani ya aina yake na kuufanya ukumbi huo utawaliwe na shamrashamra nyingi.


Vibao “Anajua Kupenda”, “Jicho la Mungu Halilali” pamoja na “Nataka Jibu” ni kati ya nyimbo zilizoiongezea msisimko zaidi shoo hiyo. Pata picha 10 za namna mambo yalivyonoga siku hiyo.
 Mashabiki wenye furaha wakiwa katikati ya ukumbi huku mvua kubwa ikikung'uta
 Safu ya waimbaji wa Jahazi Modern ikitoa raha kwa mashabiki
 Mwimbaji Prince Amigo akisherehesha kama kawaida yake
 Mishi Mohammed akipagawisha
 Hapa Shomari Zizou akicharaza gitaa la besi kwa utulivu
 Mwimbaji fatma Kassim akimwaga raha kwa sauti yake mororo ya kumtoa nyoka pangoni
 Jumanne Ulaya akicharaza nyuzi za gitaa la Solo huku akitabasamu
 Mariam BSS akiimba kwa hisia kali
 Ally Jay akipapasa kinanda kwa madoido ya hali ya juu
Mwasiti Kitoronto hapa akifanya yake jukwaani mbele ya mashabiki wao

No comments