Habari

PICHA 11: JAHAZI MODERN TAARAB YAILIPUA CHECK POINT KIGOGO FRESH… usiku huu kurejea rasmi Travertine Hotel

on

USIKU huu Jahazi
Modern Taarab wanatarajia kuanza rasmi shoo yao ya kila wiki katika siku za
Jumapili, kwenye kiwanja chao cha nyumbani cha Travertine Hotel, Magomeni Sheli
walipopasusa tangu mwishoni mwa mwaka jana.

Lakini kabla
ya shoo hiyo, jana Jumamosi vijana hao wanaoongozwa na Prince Amigo waliivamia
Kigogo Fresh, Chanika na kupiga shoo ya shibe na zifuatazo ni picha 11 za namna
mambo yalivyokwenda ndani ya ukumbi wa Check Point.
 Mpapasa kinanda Ally Jay akiwajibika kwa umakini kuwapa raha mashabiki wa Check Point
Mwimbaji Fatma Kassim akiimba kwa pozi za aina yake 

 Mcharazaji Gitaa la Solo, Hemed Emelaa akiwa kazini
 Aboubakar Soud “Amigo” akifanya yake jukwaani
 Hapa Jumanne Ulaya akicharaza nyuzi kama kawaida yake
 Mwimbaji chipukizi Aisha Kais akiburudisha 
 Hapa vidole vya Mazoea navyo vinapapasa kinanda na kuleta raha kwa mashabiki
Mwasiti Kitoronto akiwakoleza mashabiki kwa wimbo wake mpya wa “Nataka Jibu”
Emelaa akiwa amesimama barabara kwenye u MC
  Mwimbaji Mish Mohammed nae akitoa uhondo kwa mashabiki
Shomari Zizou akiliungurumisha gitaa lake la besi

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *