Habari

PICHA 20: MASHAUZI CLASSIC WALIVYOKONG’OTA SHOW YA ‘LEVO’ ZINGINE NEXT DOOR JANA USIKU

on

Ukisikia show ‘classic’ ndio kama hizi. Naam, Mashauzi Classic jana
usiku walitandika show ya levo zingine ndani ya club ya kimataifa Next Door
Masaki jijini Dar es Salaam.
Hivi ndiyo mapambano ya kuusukuma mbele muziki wa taarab yanavyotakiwa
kufanyika – kuipeleka taarab ushuani kwenye kiingilio cha buku 10 huku kinywaji
cha bei rahisi kabisa kikiwa ni soda ya shilingi eflu tatu – na si kuipeleka taarab
chini kwenye show za bure,  kiingilio
kinywaji chako.
Mandhari ya Next Door si ya mchezo mchezo, ukijitosa mle unaweza
ukajisahau na kudhani uko mamtoni na hapo ndipo utakapokubali kuwa sasa taarab
imepelekwa katika levo zingine.
Show ya jana iliyokuwa maalum kwaajili ya kusherehekea Siku ya
Wanawake Duniani, ilizizima kwa uhondo wa burudani yenye akili kutoka kwa
Mashauzi Classic huku kama kawaida Isha Mashauzi akiwa nyota wa mchezo.
Muziki mtamu ukasikika kwenye ‘sound’ ya maana ya ukumbi huo mithili
ya muziki unaotoka kwenye CD.
Clouds TV walikuwepo kwenye show hiyo ambayo pia ilikuwa na nafasi ya
kusherehekea miaka mitano ya kipindi cha TV cha Ng’ari Ng’ari kinachoongozwa na
Sakila Lioka (Mama wa Dawa Yao).
Mastaa kibao wa kike na wa kiume wakaipamba show hiyo iliyosindikizwa
na ngoma ya Kibao Kata.
Pata picha 20 za onyesho hilo huku ukikumbushwa kuwa Mashauzi Classic
wanapatikana Next Door kila Jumatano.
 Kibao Kata wakisindikiza show ya Mashauzi Classic
 Kibao Kata wakiendelea na makamuzi 
 Hashim Said jukwaani
 Isha Mashauzi akiwapa raha mashabiki wake
 Isha Mashauzi kwenye steji
 Isha akiimba Nani Kama Mama
 Kali Kitimoto kwenye kinanda
 Kutoka kushoto ni Hellen Kazimoto boss wa Next Door, Najma Love wa Star TV na Sakina Lioka wa Clouds TV
 Wadau damu wa Mashauzi Classic Allan (kushoto) na Kirikuu wakiwasili Next Door
 Rajab Kondo akilikung’uta bass
 Mchekeshaji Idrissa Makupa (Kushoto) naye alikuwepo
 Mandhari ya Next Door kwenye show ya Mashauzi Classic
 Ukumbi ulishona nyomi la kufa mtu
 Isha akiimba kwa hisia kali
 Saida Ramadhan akiimba “Pendo la Ukakasi”
 Isha na Sakina Lioka kwenye red carpet 
 Kutoka kushoto ni wadada wenye nyota zao MC Zipompa, Hidaya Njaidi, Najma Love, Sakina Lioka, Isha Mashauzi na MC Jojoo
 Waimbaji wa Mashauzi Classic jukwaani
Hidaya Njaidi, MC Zipompa, Sakina Lioka na MC Jojoo walifika kumsapoti Isha na bendi yake

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *