Habari

PICHA 21: MASHAUZI CLASSIC YAITIKISA MANGO GARDEN “USIKU WA THAMANI YA MAMA”

on

Kwa ukame wa pesa mifukoni ulioshamiri hivi sasa, ni nadra sana kuuona
kumbi za starehe zikipata ‘mafuriko’  ya
mashabiki, lakini hilo jana liliwezekana ndani Mango Garden Kinondoni jijini
Dar es Salaam.
Ilikuwa ni katika onyesho maalum la Mashauzi Classic lililopewa jina
la “Usiku wa Thamani ya Mama” ambalo lilinona vizuri.
Onyesho hilo ambalo halikuwa na fujo ya matangazo ya radio wala TV,
likashona watu watu wa nguvu kinyume na matarajio ya wengi.
Ilikuwa show fulani ya kutakata, Isha Mashauzi kama kawaida yake
akauteka ukumbi wa Mango Garden na kuwafanya mashabiki wavisuse viti vyao na
kujazana kwenye ‘dancing floor’ kwa muda wote aliokuwa akiimba.
Isha alikamua burudani mfululizo kuanzia saa 6:45 usiku hadi saa 8
akitesa na nyimbo kali kama “Nani Kama Mama”, “Tugawane Ustaarabu”, “Mama Nipe
Radhi” na “Thamani ya Mama” kabla ya kuwapisha Kibao Kata waliokuwa
wasindikizaji pekee katika onyesho hilo.
Mambo yakanoga zaidi pale Isha alipotoa zawadi mbali mbali kwa
mashabiki waliofika ukumbini na mama zao.

Tupia macho picha 21 za onyesho
hilo.
 Asia Mzinga jukwaani
 Hashim Said katika ubora wake
 Isha Mashauzi akiimba Nani Kama Mama
 Kali Kitimoto kwenye kinanda chake
 Kibao Kata wakifanya yao
 Ni wasaa wa Kibao Kata
 Isha Mashauzi Queen of the Best Melodies
 Mwandishi Robi Chacha (kushoto) akiwa na mdau Mathew Kawogo
 Isha akipokea nyekundu nyekundu kutoka kwa mdau Maiko (aliyewahi kuwa meneja wa Akudo na Malaika Band), hii ni baada ya Isha kuimba kipande cha Christian Bella ambapo alijukuta akitunzwa laki moja za papo kwa papo
Maiko, hakuishia kwa Isha, akamzawadia kila msanii mwekundu wa msimbazi
 Aisha ingizo jipya ndani ya Mashauzi Classic
Waimbaji wa Mashauzi Classic
 Hivi ndivyo mashabiki walivyokuwa wakipagawa na Mashauzi Classic jana usiku
 Isha Mashauzi
 Rahma Amani akiimba moja ya nyimbo za Mashauzi Classic
 Isha Mashauzi akitoa zawadi kwa mashabiki waliokwenda Mango na mama zao
Isha katika picha ya pamoja na mashabiki waliojishindia zawadi
Mathew Kawogo hakuweza kujizuia kwenda kumtunza Isha Mashauzi

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *