PICHA 8: MSONDO NGOMA YAJA KISASA ZAIDI …YAWAPA BIMA ZA AFYA WASANII WAKE


Wakati Msondo Ngoma ikijiandaa kuachia nyimbo mbili mpya kali sana, bendi hiyo imekuja na jambo la ‘mbolea’ zaidi la kuwaunganisha wasanii wake kwenye mfuko bima ya afya.

Hatua hiyo itawapunguzia kwa kiasi kikubwa gharama za matibabu wasanii wa Msondo ambao sasa watachangia 76,000 tu mwaka na kutibiwa bure katika kipindi chote hicho.

Leo mchana Msondo Ngoma ilifanya tafrija ya mlo wa mchana katika Hotel ya National iliyoko Chang’ombe jijini Dar es Salaam na kukabidhi kadi za bima ya NHIF (Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya) kwa wasanii wake wote. 

Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Musiki Tanzania John Kitime.

Shuhudia tukio hilo ndani ya picha zifutazo.
 Wasanii wa Msondo Ngoma wakionyesha kadi zao za NHIF
 Ridhwani Pangamawe akipokea kadi yake
 Pangamawe akionyesha kadi yake
Romario na kadi yake
Hassan Moshi naye pia akionyesha kadi yake ya NHIF
Jonh Kitime (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na viongozi wa Msondo wakati wa hafla ya kukabidhi kadi za NHIF kwa wasanii wa Msondo
Wasaa wa mlo wa mchana kwa wasanii na viongozi wa MsondoNo comments