PANAPO majaaliwa, Jahazi Modern taarab wataingia kambini katikati ya wiki ijayo kupika vibao visivyopungua vinne kwa ajili ya albamu yao ijayo, kikiwemo "Love Stori" cha bosi wa bendi hiyo, Prince Amigo.

Tayari Jahazi Modern inayosumbua vilivyo katika miondoko ya mipasho Bongo imeshatanguliza nondo zake mbili ambazo ni ‘Jicho la Mungu Halilali’ pamoja na ‘Nataka Jibu’.

Mkurugenzi wa muziki wa bendi hiyo, Ally Jay ameitonya Saluti5 kitakachofuata baada ya kukamilika kwa vibao hivyo, ni kuvirekodi na kuvisambaza kwenye vituo mbalimbali vya radio na mitandao ya kijamii.

“Baadhi ya nyimbo tutakazoingia nazo kambini ni "Love Stori" itakayoimbwa na Prince Amigo na "Utasema na Kisogo" inayotarajiwa kuimbwa Leyla Rashid, huku Mariam BSS, Mishi Mohammed na Fatma Kassim,” amesema Ally Jay.


Aidha, amesema kuwa albamu yao hiyo aliyoisifu kwa kusema kuwa itakusanya vibao moto wa kuotea mbali, itazinduliwa baada ya sikukuu ya Eid El Fitr ya mwaka huu.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac