RASHID PEMBE AMPIGIA CHAPUO BADI BAKULE VIJANA JAZZ BANDMPULIZA Saxaphone wa zamani wa Vijana Jazz Pambamoto, Rashid Pembe amemtaja mwimbaji Badi Bakule kuwa ni kati ya watu muhimu ambao wangeweza kuleta mabadiliko makubwa kama angetua katika bendi hiyo.

Akiongea katika kipindi cha Afro Tz cha Radio One, kinachoruka hewani kuanzia Jumanne hadi Alhamisi kila wiki chini ya mtangazaji Rajab Zomboko, Pembe alisema kuwa Bakule angeweza kuja kuziba pengo la marehemu Jerry Nashon “Dudumizi”, kutokana na uimbaji wao kushabihiana.
 
“Kinachotakiwa hapo ni kwanza wanamuziki wenyewe waliopo sasa kuwa tayari kuyapokea mapinduzi, kwa kubali kuwaleta wanamuziki ambao wamewazidi uwezo, kama ambavyo kipindi kile sisi tulivyowavuta Suleiman Mbwembwe, Rahma Shari na Dudumizi ili kuziba pengo la Maneti,” amesema. 
 
Aidha Pembe amesema kuwa, pamoja Bakule, pia bendi hiyo ingefanya utaratibu wa kuwarudisha wanamuziki wakle wa zamani wanaong’ara sasa kwenye bendi nyingine, kama vile wapiga ala Miraji Shakashia (gitaa la Solo), James Mawila na Juma Choka (Drums).

No comments