RASHID PEMBE ASHAURI VIJANA JAZZ IZIBOMOE SIKINDE, MSONDO NA TWANGA ILI KUJIIMARISHA

MKONGWE wa Saxaphone, Rashid Pembe “Professor” amesema kuzibomoa bendi tatu za Mlimani Park “Sikinde”, Msondo Ngoma na Twanga Pepeta, kwa kunyofoa wanamuziki kuanzia wawili kila upande, ndio njia pekee inayoweza kuirejesha bendi ya Vijana Jazz kwenye ubora wake.

Akizungumza kwenye kipindi cha Afro Tz kilichoruka hewani Jumanne hii katika Studio za Radio One Sterio chini ya mtangazaji Rajabu Zomboko, Pembe amesema kuwa hiyo itafufua hamasa za washabiki kwenye bendi hiyo inayomilikiwa na Umoja wa Vijana.

“Ukishazitia ufa bendi hizo kwa kuwachukua baadhi ya wanamuziki wake tegemeo, mashabiki nao sasa watakuwa na hamu ya kutaka kujua ujio mpya wa Vijana Jazz baada ya usajili huo na ndipo chati itakapopanda tena,” amesema Pembe.


Amesema anaamini hiyo itakuwa ndio dawa kwa kile alichodai kwamba, pamoja na sababu ya viongozi wa Umoja wa Vijana walioko sasa kukosa mshituko kwa bendi yao, lakini Sikinde, Msondo na Twanga pia ndio zimechangia kwa kiasi kikubwa kuiporomosha Vijana Jazz. 

No comments