REAL MADRID, BARCELONA KUPAMBANA MAREKANI JULAI 29

MIAMBA miwili ya soka nchini Hispania, FC Barcelona na Real Madrid zitacheza kwa mara ya kwanza nchini Marekani.
Taarifa iliyotolewa nchini humo inasema kwamba pambano hilo ni sehemu ya International Champions Cup (ICC) na litapigwa mwezi Julai mwaka, huu.

Hii ni mara ya pili kwa El Classico kuchezwa nje ya Hispania. Miaka 34 iliyopita Real Madrid na Barcelona walikutana nchini Venezuera.


Timu hizi zitakutana Julai 29, mwaka huu na pambano hilo linasubiriwa kwa hamu na wengi kama kivutio kwa watu wengi duniani kufika katika mji wa Miami ambapo ndipo pambano hilo litapigwa

No comments