REAL MADRID WATISHIA KUZIRARUA NYAVU ZA CHELSEA

KAMA jamaa hawatajipanga vizuri basi lazima wakubali kwamba kuna siku wataumbuka tena kiurahisi zaidi.

Na hizi zinaweza kuwa habari mbaya sana kwa Chelsea ambayo inatajwa kwamba iko katika wakati mgumu baada ya Real Madrid kutishia kumsajili kipa wake namba moja.

Na habari zinasema kwamba kwa sasa hakuna njia nyingine isipokuwa Chelsea kumpa mkataba utakaokuwa na dhamana ya pauni 200,000 kwa wiki mlinda mlango Thibaut Courtois ili kuepuka harakati za Real Madrid kumnasa.

Gazeti moja nchini Hispania limeandika kwamba linafahamu kila kinachojiri kwamba Real Madrid hawana mtu wanayemuwinda katika nafasi hiyo zaidi ya Mbelgiji huyo.


“Kama Chelsea hawana muda wa kulitafakari hili wanaweza kujikuta baadae hawana muda pia wa kumzuia kipa huyo kuondoka,” limeandika gazeti hilo.

No comments