REAL MADRID YAKANUSHA TETESI ZA USAJILI WA MATEO KOVACIC

KLABU ya Real Madrid imekanusha juu ya tetesi za usajili wa nyota wake Mateo Kovacic na kuzipasha timu zinazomwania kwa kuwaambia hawana mpango wa kumuuza kwa gharama yoyote.

Kabla ya kauli ya klabu hiyo ya La Liga, Mateo alivumishiwa kutakiwa na Manchester United ambao wanapambana kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha mzunguuko wa pili wa Ligi ya primier.

Kocha wa mashetani hao, Jose Mourinho amekuwa akimzungumzia kiungo huyo mwenye uraia wan chi mbili za Austria na Croatia, kama sehemu ya mkakati wake wa kukisuka kikosi cha kusaka heshima na ubingwa kwa misimu ijao.

Lakini kocha Zinedine Zidane amenukuliwa na Sky Sports akisema kuwa klabu yake haina mpango wa kumuuza kiungo huyo licha ya kupokea ofa kutoka katika timu mbalimbali ikiwemo Manchester United.


Mara baada ya taarifa za kiungo huyo kuamua kutua Old Trafford, kocha Zidane ameachana na mpango wake huo na kutangaza rasmi kutouzwa kwa Mateo Kovacic.

No comments