REHEMA TAJIRI AENDELEA KUTIA MSISITIZO "TX MOSHI WILLIAM ALIKUWA RAFIKI TU"



MWANAMUZIKI mahiri wa kike wa miondoko ya dansi Bongo, Rehema Tajiri ameendelea kusisitiza kuwa hakuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu Tx Moshi William aliyekuwa mkali wa sauti ndani ya Msondo Ngoma Music Band.

Akiongea wiki hii katika kipindi cha Afro Tz cha Radio One Stereo chini ya mtangazaji Rajab Zomboko, Rehema alisema kuwa, baadhi ya wamekuwa wakiipotosha jamii kwa kueneza uvumi huo wenye lengo la kumchafulia jina.

“Hatukuwa na mahusiano mengine zaidi ukiondoa kwamba Tx Moshi alikuwa mwalimu wangu katika muziki, aliyenisaidia sana hasa katika kuandaa wimbo wangu wa “Sumu ya Ndoa”, ulionipa umaarufu mkubwa,” alisema Rehema.
 
Alisema kuwa, waliheshimiana na nguli huyo ambapo alifika nyumbani kwake muda wowote na aliaminiwa hadi kwa aliyekuwa mkewe, Asha mwana Seif ambaye naye kwa sasa ni marehemu.

No comments