REHEMA TAJIRI ASEMA ILIBAKI KIDOGO WIMBO WAKE WA "SUMU YA NDOA" UIMBWE NA LUIZA MBUTU

MWIMBAJI wa muziki, Rehema tajiri amefichua kwamba wimbo wake uliompatia jina kubwa wa “Sumu ya Ndoa” aliutunga ili ampe Luiza Mbutu wa African Stars wa Twanga kuimba, kabla hajaamua kuufanyia mazoezi yeye mwenyewe.

Akiongea hivi karibuni kwenye kipindi cha Afro Tz cha radio One, Rehema alisema kwamba alitaka kumpa Luiza wimbo huo kutokana na kuwa mume wake (wakati huo) marehemu Sahau Kambi alikuwa akimzuia kujihusisha na masuala ya muziki.


“Ule wimbo ni kisa cha kweli kwani niliutunga kutokana na matatizo ya ndoa yangu na Sahau kambi kipindi kile na niliamua kuutunga kwa hisia zote na kukusudia kumpa Luiza, ila baadae niliamua kuurekodi mwenyewe baada ya kujiona niko huru,” alisema.

No comments