REKODI YA KOCHA WA YANGA KWA WAARABU YAWASHITUA WANIGERIA

KOCHA wa Yanga, George Lwandamina anataka kuleta mshtuko nchini Algeria kufuatia rekodi yake nzuri dhidi ya timu za Uarabuni.

Yanga ambayo inashiriki kombe la shirikisho ikipangwa kucheza dhidi ya MC  Algers yaAlgeria kocha wao ameonekana kuwa na rekodi bora akipoteza mechi moja tu katika timu tatu za Uarabuni.

Katika hatua za mtoano Lwandamina akiwa na Zesco ameifunga Al Ghazal ya Sudan mechi zote mbili akiwapiga 2-0 nyumbani kasha kuwachapa 1-0 ugenini.

Hakuishia hapo katika hatua ya makundi ya ligi  mabingwa alikutana na timu mbili za Uarabuni alizopangwa nazo timu moja ambapo aliwafuga Al Ahly ya Misri nyumbani 3-2 kisha kutoka nao sare ya mabao 2-2 ugenini.


Lwandamina alikuta tena na Wydad Casabranca ya Morocco ambapo alitoka nao sare nyumbani ya bao 1-1 kisha kufungwa mabao 2-0 ugenini ukiwa ndio mchezo pekee kupoteza dhidi ya timu za Uarabuni uku akifanikiwa kutinga hatua na nususu fainali na kutolewa na mabingwa watetezi msimu huu Mamelod Sundown ya Africa kusini.

No comments