ROBERT LEWANDOWSKI KUMFUATA PEP GUARDIOLA MANCHESTER CITY

STRAIKA Robert Lewandowski ameweka bayana dhamira ya kutaka kuachana na Bundersliga, huku akishindwa kusema wazi kuwa ataondoka lini.

Lakini taarifa za ndani zinasema kuwa, Straika huyo anasemekana ameweka malengo ya kutaka kukipiga katika Ligi ya Premier, hasa kutokana na kutaka kubadilisha mazingira.

Taarifa za uwezekano wa kuhama kwa mfumania nyavu huyo zinakuja kufuatia gazeti la Telegraph kuanika tetesi za hivi karibuni za kutakiwa na klabu za Manchester City, Barcelona na Manchester United.

Hata hivyo kuna tetesi kuwa Lewandowski ana asilimia kubwa za kumfuata bosi wake wa zamani, Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City na kwamba taarifa za hivi sasa kutangaza kuondoka Bayern ni mwanzo tu wa kukamilika dili hilo.

Pep ambaye ni kocha wa sasa wa matajiri wa jiji la Manchester, ameweka bayana azma ya kutaka kuendelea kukisuka kikosi chake ifikapo kipindi cha usajili cha majira ya kiangazi.

Wakala wa Lewandowski, Cezary Kucharski amenukuliwa akikiri kuwa tayari ameetaarifiwa juu ya utajiri wa kuondoka kwa straika huyo aliyekuwa Bayern akitokea kwa Dotmund misimu miwili iliyopita.

Kucharski alibainisha pia kuwa, mchezaji huyo tayari ameonesha dhamira ya kuhama kutoka bundersliga na huenda akatua Englnd au Hispania.

Akinukuliwa zaidi wakala huyo alisema; “Ninafikiri inaweza kuwa ni ofa ya hali ya juu kwake kuhama kutoka Bayern, lakini haitakuwa chini ya euro mil 50.”

“Robert ni kati ya wachezaji walio na thamani kubwa kwa sasa, ambao wapo sokoni kwa ajili ya msimu huu wa usajili wa majira ya kiangazi.”


“Kila timu inamtaka Robert kwa gharama inayofanana na hadhi aliyonayo kwasababu ana uwezo mkubwa wa kufunga magoli hasa katika mazingira tofauti.”

No comments