ROY KEANE AMSHUKIA VIBAYA MOURINHO, AMTAKA APUNGUZE MALALAMIKO YA KIPUUZI


Roy Keane amemnanga Jose Mourinho kwa malalamiko yake juu mbanano wa ratiba na kusema pengine Manchester United ni kubwa kuliko kocha huyo. 
Mourinho amelalamika kuwa ratiba imebana sana hususan baada ya kuwapoteza Paul Pogba na Daley Blind walioumia Alhamisi usiku katika mchezo wa Europa League dhidi ya Rostov ya Urusi.
Baada ya Manchester United kusonga mbele na kutinga hatua ya robo fainali, sasa klabu hiyo inaweza ikajikuta inacheza mechi 17 kabla msimu haujaisha na kuna wakati italazimika kucheza kila baada ya siku tatu.
Roy Keane akasema: "Sijawahi kusikia upuuzi wa namna hii katika maisha yangu. Kwanini tupoteze muda kusikiliza upuuzi wa kiasi hiki, alihoji Roy Keane baada ya kusikia malalamiko ya Mourinho.
"Anazungumza vitu visivyo na tija. Ni kocha wa Manchester United, moja ya klabu kubwa duniani, kikosi kipana alichonacho, wachezaji alionao ...na bado analalamikia kuhusu ratiba.
"Pengine klabu ni kubwa kuliko yeye, hawezi kukabiliana na majukumu yake mchezoni. Mechi zipi? hata timu ya akiba ya Manchester United ingeweza kushinda mchezo huu".

No comments