Habari

SAMIR NASRI AMCHANA GUARDIOLA… asema ni kigeugeu aliyekataa kumsikiliza kuhusu kubaki Man City

on

KUMBE Samir
Nassri aliambiwa na kocha wake, Pep Guardiola hasiondoke lakini straika huyo
aliamua kusepa!
Alipoulizwa kwanini
aliamua kuondoka, Samir alijibu: 
“Kocha Pep ni mtu kigeugeu na haaminiki, hivyo
isingekuwa rahisi kwangu kumkubalia kubaki maana nisingekuwa na namba ya kudumu.”
“Niliamua
hilo kwa maslahi ya kiwango changu cha soka kwasababu nilikuwa nahitaji
kuendelea kucheza katika kikosi cha kwanza.”
Kauli hii ya
Nasri inakuja wakati huu ambapo anakaribia kutiomiza mwaka mmoja ndani ya
kikosi cha timu yake ya sasa ya Sevilla inayoshiriki La Liga nchini Hispania.
Katika mazingira
yasiyo ya kawaida, Nasri alimeza mate ya akili na kumkatalia kocha wake huyo
kwa kile alichodai kuwa uwezekano wa namba katika kikosi cha Manchester City ni
mdogo.
Nasri aliingia
katika kapu la wachezaji ambao tangu kocha Guardiola atue Manchester City
wamekuwa hawana nafasi katika kikosi cha kwanza.
Wachezaji hao
ni pamoja na Joe Hart, Wilfried Bony, Eliaquim Mangala na Jason Denayer ambao
ni kama walionyeshwa mlango wa kutokea mapema.
Nasri mwenye
umri wa miaka 30, alisema: “Guardiola alitaka nibaki City kwa ahadi ya kuwa
nitapata namba kikosini.”
“Lakini
nilimkatalia nikitambua kuwa kauli yake haikuwa na ukweli halisi.”
“Mimi ni
mchezaji na ninahitaji kucheza siku zote ili kulinda kiwango change kisishuke.”

“Nimejiunga
Sevilla ikiwa ni timu ambayo ni kama familia yangu. Nina uhakika wa kucheza
nikiwa hapa.”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *