SHEREHE YA KUZALIWA YA MAMA YAKE ALI KIBA YAZUA MASWALI MENGI KWA MASHABIKI

MWISHONI mwa wiki iliyopita mama wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba alizaliwa na kusherehekea miaka kazaa ya kuzaliwa lakini licha ya kufanyiwa pati, mashabiki waliachwa na maswali mazito.

Moja ya swali lililoibuka kwenye siku hiyo ya kuzaliwa ni kwa nini wasanii wanaofanya vyema wote hawapo karibu na baba zao wazazi.

Wengi walihoji huwenda baba wazazi wa wasanii hao wametangulia mbele za haki lakini hata wale waliopo hai wamekua hawaonekani.

Shabiki Mohammed Msuya aliandika kwenye ukurasa wa Ali Kiba; "Mimi naomba kuuliza kwani hawa wasanii hawana baba jamani mbona kila siku ni picha za wakina mama ila samahani kama nitakuwa nimekwaza watu."

Licha ya swali hilo msanii huyo hakujibu na kufanya kuulizwa mara kwa mara huku wengi wakiomba ufafanuzi zaidi.


Lakini si Ali Kiba wala wale mashabiki wanaojiita team Kiba walishindwa kujibu swali hilo na kuzidi kuacha maswali.

No comments