SHILOLE ASEMA HATOI KIKI BILA PESA …kiki za kizembe tupa kule


Staa wa muziki wa kizazi kipya Shilole (Shishi Baby) amesema hana muda wa kutoa kiki za kizembe bali anatoa kiki kwa pesa.

Kiki ni mfumo wa kutengeneza stori za bifu au skendo ili kujiongezea umaarufu kupitia jina la mtu mwingine.

Akiongea katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM mchana huu, Shilole akasema kiki anazotoa ni za pesa, kinyume na hapo hana muda huo.

“Mimi ukitaka kiki basi tunaandikishiana mkataba unanilipa changu kisha nakupa kiki, kutoa kiki za kizembe zembe I can’t,” alisisitiza Shishi Baby.

No comments