SIR ALEX FERGUSON ATOA USHAURI WA BURE KWA JOSE MOURINHO

KIROHO safi kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amemwambia kocha wa sasa wa mashetani Wekundu hao, Jose Mourinho kama anataka kuongeza wachezaji kikosini anatakiwa kuacha kabisa kufanya usajili wa kuangalia majina.

Amesema, anapaswa awe mbunifu wa kuangalia aina ya wachezaji wanaoweza kulelewa ndani ya Unted ili waje kuwa nyota wa baadae.

Ferguson aliyasema hayo katika kipindi hiki ambacho nyota Paul Pogba hajaanza kuonyesha mafanikio yaliyotarajiwa na wangi tangu asajiliwe kwa gharama kubwa.

“Ninaweza nikamwambia jambo moja kocha Jose Mourinho kuwa, kama atataka kufanya usajili katika dilisha la kiangazi, basi aachane na usajili wa majina makubwa.”

“Badala yake angalie wachezaji walio na vipaji, lakini wa umri mdogo.”

“Mimi nilifanya hivyo kwa wachezaji wengi, akiwemo Ryan Giga Rio Ferdinand, Cristian Ronldo na hata Wayne Rooney. Ingawa walikuwa hawana majina, lakini walikuja kuwa tegemeo katika timu.”

“Kisha kocha kama wa United lazima aangalie utamaduni wa soka la Engand ambalo ni la kujali zaidi wachezaji wanaoweza kudumu kikosi kipindi kirefu,” alisisitiza Ferguson.


No comments