Habari

SIR ALEX FERGUSON KUREJEA MANCHESTER UNITED JUNI 4, MWAKA HUU

on

KOCHA Sir
Alex Ferguson ndiyo nembo iliyoko nyuma ya mafanikio ya Manchester United kuanzia
mwaka 1986 hadi 2013 aliwapa karibia kila kombe kuanzia Uingereza Ulaya na
Dunia nzima.
Tangu baada
ya Ferguson kuondoka timu hiyo imekuwa ikiyumba huku makocha wawili waliomfuata
David Moyes na Luis Van Gaal wakishindwa kuwapa kile wanachotaka, huku kocha
wao wa sasa Jose Mourinho kidogo akianza kuwafuraisha.
Tayari
mashabiki wa Manchester United dunia nzima walianza kupiga kelele wakitaka
Ferguson arudi kutetea Jahazi lao linaonekana kuzama kabla ya Morinho kuanza
kuwainua.
Lakini sasa
kiu ya mashabiki wengi wa Manchester United ya kumuona Ferguson akiwa kwenye
benchi la Old Traffold kama kocha inaelekea kutimia, Ferguson atarudi kama kocha wa United Juni 4, mwaka huu.
Ferguson
ambaye hadi anastaafu alishawapa United jumla ya makombe 26, atakuwepo kwenye
mchezo maalum kwa ajili ya kiungo wa Manchester
United, Michael Carrick.
Ferguson
katika mchezo huo atakuwa kocha wa wachezaji wa zamani wa Mancherster United.
Ferguson
atakuwa kocha wa kikosi cha wachezaji wa zamani wa United ambao watacheza na
timu ya Carric.

Pengine hii
itawavutia sana washabiki wa Manchester United, kwani toka Ferguson  atangaze kuustafu hawajawai tena kumuona
akisimama nje ya uwanja kama kocha. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *