KUBAKI kwa kocha George Lwandamina sio kwa akili ya kutaka kupumzika na kwamba anatafuta mshambuliaji wa maana atakayeongeza kasi ya safu ushambuliaji.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema Lwandamina anafanya siri kubwa katika msako wa mshambuliaji huyo ambaye ametaka asajiliwe kuzima ukame wa mabao katika kikosi chake.

Bosi mmoja ya Yanga amesema Lwandamina anataka kuhakikisha anamnasa mshambuliaji huyo ambaye inaelezwa anamalizia mkataba wake katika klabu moja ya Ulaya ili aje kujiunga na Yanga.

Kigogo huyo alisema mbali na mshambuliaji pia kocha huyo anataka kutafuta kiungo mchezeshaji katika kujiandaa na kuondoka kwa Haruna Niyonzima ambaye yupo katika mkao wa kutimkia Cyprus.

”Unajua mnamuona yule kocha kama hajui anachofanya, amebaki Zambia kwa kazi maalum anatafuta mshambuliaji ambaye ataongeza kasi katika safu yetu ya ushambuliaji,” alisema bosi huyo.


“Kuna mshambuliaji anamtaka ametuonyesha tumemkubali ni mtu anayejua kufunga kwa sasa anamalizia mkataba wake Ulaya anataka kurudi Afrika sasa anataka kumshawishi aje hapa lakini pia anatafuta kiungo mchezaji."
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac