SNOOP DOGG KUACHIA ALBAMU MPYA IITWAYO "NEVA LEFT" MWEZI MEI MWAKA HUU

RAPA mkongwe, Snoop Dogg ameweka wazi kwamba amekamilisha albamu mpya na kwamba ataiachia Mei, mwaka huu.

Msanii huyo aliitaja kazi yake hiyo mpya kuwa ni “Neva Left” na akasema itakapotoka itabamba kuliko maelezo.

Snoop Dogg alibainisha hayo kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter na Instagram akisema zitasikika sauti za wakali kadhaa.

Alisema, baada ya ukimya wa muda mrefu sasa ameamua kuwapa mashabiki wake kitu walichokikosa kwa muda mrefu na akaifagilia sana albamu hiyo.

No comments