Habari

STEVEN GERRARD AIVULIA KOFIA BARCELONA, NEYMAR …asema hajawahi kuona soka kama lile

on

Nyota wa zamani wa England na Liverpool Steven Gerrard amesema amekoshwa na soka la Neymar na Barcelona kwa ujumla wake kufuatia mechi yao ya maajabu dhidi ya PSG Jumatano usiku.

Katika mechi hiyo ya Champions League, Barcelona iliyokuwa inadaiwa 4-0, ikaibuka kijogoo Nou Camp kwa ushindi wa 6-1 na hivyo kusonga mbele kwa jumla ya magoli 6-5.

“Wachezaji wa daraja la juu (World class players) huleta maajabu katika muda muafaka” alisema Steven Gerrard wakati akichambua mchezo huo sambamba na Rio Ferdinand na Michael Owen.
“Luis Suarez na  Lionel Messi hawakuwa tishio sana, lakini Neymar alionyesha soka la hali ya juu, ni moja ya viwango bora ambavyo sikuwahi kushuhudia hapo kabla,” aliongeza Gerrard.

Neymar ambaye alikuwa hazuiliki, alifungia Barcelona bao la la nne kwa free-kick ya mbali dakika mbili kabla mpira haujaisha, kisha akaifungia  la tano dakika ya 90 kwa penalti kabla hajasaidia kutoa pasi kwa Sergi Roberto aliyekwamisha bao la mwisho dakika za majeruhi. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *