TAMBWE, MSUVA WAONYWA KUACHA UBINAFSI NA UVIVU ILI KUIBEBA YANGA

MSHAMBULIAJI mahiri kutoka Burundi, Amissi Tambwe na Winga Simon Msuva wametakiwa kuibeba timu hiyo kwa kufunga mabao.

Wito huo umetolewa na wanachama wa Yanga tawi maarufu la Ubungo Terminal walipozungumza na Saluti5 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam juzi.

Baadhi ya wanachama wa tawi hilo walisema, iwaapo wachezaji hao watadhamiria kufunga na kujituma kila mechi, wataipa Yanga ubingwa wa msimu huu.

“Sisi tunaamini nafasi ya ubingwa kwa Yanga msimu huu ni kubwa sana, cha msingi tu ni Tambwe na Msuva kuacha ubinafsi na uvivu,” alisema mmojawao.


Wakifafanua zaidi wanachama hao walisema iwapo wachezaji hao ambao wameonyesha uwezo mkubwa wa kufunga mabao watazitumia vizuri nafasi watakazozipata katika kila mchezo, hakuna timu ya kuizuia Yanga kwa ubingwa.

No comments