TANCUT ALMAS ORCHESTRA KUMRUDISHA KING MALUU KWENYE JUKWAA LA MUZIKI WA DANSI

TANCUT Almasi ya Iringa ndio bendi pekee ambayo mkongwe King Maluu atajipeleka na kuomba kujiunga nayo kama itafufuliwa upya, ingawaje alishaapa kutojihusisha na masuyala ya muziki wa dansi tangu mwaka 1990.

Maluu alibainisha hayo hivi karibuni katika mahojiano yake na mtangazaji Rajab Zomboko wa kipindi cha Afro Tz cha Radio One Stereo.


“Maisha pale Tancut yalikuwa ya raha sana, pesa ilikuwa nyingi, wanamuziki wote walikuwa ni wenye uwezo waliopiga muziki mkubwa… aisee ile bendi kama itarudi itanirudisha na mimi kwenye dansi,” alisema Maluu.

No comments