TANZANIA PRISONS WAJILAUMU KWA KUFANYA VIBAYA MWANZONI MWA MSIMU WA LIGI

KUTOKANA na mafanikio wanayoyapata sasa, kocha wa maafande wa Tanzania Prisons, Abdallah Mohammed amesema kuwa timu hiyo iliteleza katika mechi za mwanzoni mwa msimu.

Mohammed amesema kuwa kiwango cha timu yake kwa sasa kipo vizuri tofauti na walivyouanza msimu huu akisema hivi sasa wanacheza soka la kufundishwa na la kitimu zaidi.

Alisema, mwanzoni mwa msimu walicheza kwa kutegemea vipaji binafsi vya wachezaji, jambo ambaloliliwafanya kupata matokeo mabaya.

“Kwa kweli hivi sasa hata tukikosa matokeo lakini mashabiki wakija uwanjani wanafurahia soka letu. Kama tungeanza hivi tangu mwanzo tungekuwa katika mbio za ubingwa,” alisema.


Alisema, kwa kuwa timu hiyo inaundwa na wachezaji wengi waajiriwa wa Jeshi la Magereza, anaamini itakuwa moto wa kuoteambali msimu ujao kutokana na wachezaji hao kukaa pamoja.

No comments