THEO WALCOTT AOTA NNE BORA YA PRIMIER ARSENAL

WINGA wa Arsenal, Theo Walcott ni kama anakuja na kauli za kuwapoza nafsi mashabiki wa klabu hiyo duniani kote pale anapokuja na kauli ya kutokata tamaa juu ya nafasi ipi ambayo timu itamaliza katika msimamo wa Ligi ya England.

Katika hali ya kujiamini, Walcott amenukuliwa akisema kikosi chao bado hakiwezi kukata tamaa ya kuwemo katika orodha ya timu nne zitakazomaliza zikishika nafasi nne za juu pindi ifikapo mwisho wa Ligi ya msimu huu.

Kauli ya Walcott inakuja siku chache baada ya “The Gunners” kuondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa mabao ya jumla ya 10-1 dhidi ya Bayern Munich, matokeo ambayo yamewakasirisha wadau wengi wa klabu hiyo ambao wamekata tamaa hata ya kumaliza ikiwa ya nne.

Lakini akizungumza kwa kujiamini Walcot alisema pamoja na baadhi ya mashabiki juu ya mweneno wa timu hasa kwa kocha Arsene Wenger lakini lazima watambue kuwa Ligi bado haina mwenyewe hasa katika kinyang’anyiro cha nafasi nne za juu.

“Huwezi kuiondoa Arsenal katika mbio za ubingwa ama kati ya timu nne za kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.”


“Ninajua kuna watu hawawezi kuamini hili nilisemalo, lakini hilo ni jambo la kujidanganya kwa sababu sisi kama wachezaji tunaendelea kupambana kwa ajili ya kuhakikisha tunamaliza katika nafasi nne za juu.”

No comments