TIMU YA MAJIMAJI YASIMAMISHA WACHEZAJI WANNE KWA UTOVU WA NIDHAMU

WACHEZAJI wanne wa Maji Maji ya Songea mkoani Ruvuma, George Mpole, Peter Joseph,Yussuf Mfanyeje na Ibrahim Tende wamesimamishwa kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.

Mwenyekiti wa wana Lizombe hao Humphrey Milanzi amesema kwamba wachezaji hao wamefanya utovu wa nidhamu ambao klabu haiwezi kuvumulia.

Milanzi amesema kwamba ili liwe fundisho kwa wachezaji wengine,Uongozi umeamua kuwasimamisha wachezaji hao.
Na amesema wachezaji hao wanaweza kusamehewa iwapo tu watajirekebisha na kuomba msamaha kutokana na makosa yao.

Aidha, Milanzi alisema kwamba kwa sasa uongozi unajikita katika jitihada za kuhakikisha anainusuru timu kushuka daraja kwa kuhakikisha timu inashinda mechi sake zote saba zilizosalia za Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.


Maji Maji kwa sasa inashika nafasi ya pili kutoka mwisho katika msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza mechi 24, juu ya JKT Ruvuinayoshika mkia kwa pointi zake 20 za mechi 24 pia.

No comments