TOLINO KUMNG'OA ANDRE AYEW WEST HAM KWA PAUNI MIL 18?

KLABU ya Tolino ya nchini Italia imeweka mpango wake mezani na sasa iko tayari kuweka mezani kitita cha pauni mil 18 kwa ajili ya kumnasa straika wa West Ham United, Andre Ayew, hii ni kwa mujibu wa Sky Sports.

Straika huyo raia wa Ghana ameingia katika rada ya Wataliano hao inayotaka kuendelea kusuka kikosi chake imara kwa ajili ya kupambana kwa ajili ya ubingwa msimu ujao.

Tayari Tolino ambayo ina mlinda mlango Joe Hart kutoka Manchester City, wameteta na wakala wa nyota huyo na kwamba hata west Ham wenyewe wamethibitisha za kuweko kwa pilika kuhusiana na straika huyo.

Wakitambua hilo, Tolino wamemtengea kiungo huyo kitita cha pauni mil 18 wakiongeza dau waliloweka awali ambalo lilikuwa pauni mil 15.

“Andre Ayew anawindwa na timu nyingi za Ulaya, lakini nataka acheze katika kikosi ambacho atapata namba ya kudumu.”


“Ni mchezaji mwenye ofa nyingi, ila ni jambo la kusubiri kuona ifikapo kipindi cha usajili kikifika mwisho,” ilieleza taarifa ya klabu ya Tolino.

No comments