TORRES ACHEKELEA KUWEPO ATLETICO MADRID… asema ni mpango wa maana unaompa faraja na mambo kuendelea kumnyookea

FERNANDO Torres amesema uamuzi wake aliouchukua miaka miwili iliyopita wa kurejea katika klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid, ni mpango wa maana na anajisikia faraja kuona mambo yanaendelea kumnyookea.

Kisha, akakiri kupanda kwa kiwango chake kiasi cha kurudisha makali yake ya kupachika mabao na hata kuisaidia timu yake hiyo.

Sky Sports wameripoti kuwa Fernando Torres anajisikia furaha kuwa Madrid kuliko alivyokuwa katika klabu zote alizowahi kuzitumikia, ikiwemo Chelsea.

Torres alikuwa akikipiga kwa mkopo katika klabu ya AC Milan akiwa mali ya The Blue ya England kabla ya kuamua kurejea katika La Liga.

“Ni kama nimezaliwa upya hapa Atletico Madrid, ni wakati wangu wa kuangalia maisha mapya ya kisoka, hasa nikiamini nimerudi katika klabu iliyonipa jina na mafanikio makubwa,” alisema Torres.


“Maisha hapa ni mazuri na kiwangu kimepanda na nafurahi kuona nina namba katika kikosi cha kwanza kuliko nilivyokuwa AC Milan, haya ni matarajio yangu makubwa sasa.”

No comments