TOTO AFRICAN WAAPA KUBAKIA LIGI KUU TANZANIA BARA

KOCHA wa timu ya Toto African ya jijini Mwanza, Fulgance Novatus amejiapa kuwa timu hiyo haitoshuka daraja.

Novatus aliyeichukua timu hiyo hivi karibuni ili kuokoa jahazi lisizame, amejitapa akisema kuwa, chini yake Toto haiwezi kushuka daraja.

Alisema, anao uhakika kuwa itashinda mechi sita zilizosalia na kubakia Ligi Kuu, akisema amethibitisha uwezo kwa jinsi walivyoifunika Mbao FC wikiendi iliyopita na kuipiga mabao 2-0.

“Mimi nina uhakika chini yangu Toto haiwezi kushuka daraja, kweli kuna hali mbaya lakini tukishinda michezo yetu iliyosalia hatushuki, na hilo ndilo tutakalofanya,” alisema.


Alibainisha kuwa hivi sasa wanafanyia kazi makosa yote yaliyojitokeza katika mechi zilizopita ambayo yaliwagharimu na kwamba baada ya hapo watapata ushindi.

No comments