TOTTENHAM WAWEKA MEZANI JINA LA MLINZI WA LIVERKUSEN

TOTTENHAM Hotspurs wameweka jina la mlizi wa Bayer Liverkusen, Lukas Boeder ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika timu ya SC Paderborn 07.

Kwa mujibu wa Daily Mail, Spurs inapambana na klabu nyingine zinazowania saini ya mlinzi huyo, zikiwemo klabu nyingi za Ulaya ikiwemo Nice, Tolino na West Ham United.

Boeder amekuwa katika kiwango kizuri kwa miaka miwili iliyopita na kuwa tegemeo katika kikosi cha Bayer Liverkusen.

Mlinzi huyo amekuwa miongoni mwa wachezaji wa mwanzoni kuingia katika rada za usajili wa Spurs inayopanga kupambana kwa ajili ya kumaliza ikiwa katika orodha ya timu nne za juu katika Ligi ya premier msimu huu.

Katika kuhakikisha wanafanikisha azma hiyo, Spurs imekuwa ikimfuatilia Boeder katika baadhi ya mechi ambazo SC Paderdoln 07 wanazompanga mlinzi huyo katika kikosi cha kwanza.


Mawakala wa Tottenham wamekuwa wakisafiri mara kwa mara hadi nchini Ujerumani kwa ajili ya kujiridhisha na kiwango cha sasa cha mlinzi huyo.

No comments