TOTTENHAM HOT SPUR WAMTUPIA NDOANO MLINDA MLANGO JOE HART

UVUMI unaozagaa hivi sasa nchini England unahitaja timu ya Totten Ham Hot Spur kutaka huduma ya mlinda mlango Joe Hart ambaye kwa sasa anadakia timu ya Tolino ya Italia.

Taarifa za ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa, kocha Mauricio Pochettino ameingia katika harakati za kumwania Hart akiamini kuwa atakuwa chaguo la kwanza kikosini mwake.

Pochettino amenukuliwa akimzungumzia Hart kama chaguo la kwanza katika kikosi cha England, hivyo atakuwa na msaada mkubwa pindi akitua katika kikosi cha majogoo hao wa jiji.

Hata hivyo, kocha huyo anaamini kuwa mlinda mlango huyo ana nafasi kubwa ya kung’ara katika kikosi cha timu yoyote inayomwitaji, ingawa alikosa nafasi ya kuaminika pindi Pep Guardiola alipotua Manchester City mapema msimu huu.

Kutakiwa kwa kipa huyo na timu mbili hizo za primier kunaweza kuongeza joto la ushindi kwa ajili ya hart kwani klabu ya Borussia Dortmund ya nchini Uingereza nayo imeingia vitani kusaka saini yake.


Hart alijikuta akikosa namba katika kikosi cha Pep na kufanya ashawishike kulinda kiwango chake kwa kuhamia katika kikosi cha Tolino kinachoshiriki Ligi ya serie A ya nchini Italia.

No comments