TWANGA PEPETA KUTAMBULISHA NYIMBO MPYA TATU ALHAMISI HII COCO BEACH


The African Stars Band “Twanga Pepeta” Alhamisi hii watakuwa na onyesho maalum la kuwasikilizisha mashabiki (Listening Party) nyimbo zao mpya tatu.

Onyesho hilo litafanyika katika ukumbi wa Coco Beach, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Twanga Pepeta Asha Baraka ameiambia Saluti5 kuwa nyimbo hizo ni “Prison Love”, “Yamepita” na “Kalunde” ambazo zote zimepigwa katika miondoko ya kisasa zaidi kulinganisha na nyimbo za zamani za bendi hiyo.

“Prison Love” ni utunzi wa Khalid Chokoraa huku “Yamepita” ikiwa ni kazi ya Haji Ramadhan (Haji BSS) wakati “Kalunde” umetungwa na Twanga Digital.

Twanga Digital ni kundi la waimbaji chipukizi …vijana wanne damu mpya kabisa iliyoingizwa kundini wakitokea taasisi ya Mkubwa na Wanawe ya Said Fella.

Katika nyimbo zote hizo tatu, ladha ya Twanga Digital itapatikana ndani yake.

No comments