UJERUMANI YAKANUSHA KUWA NA MPANGO WA KUACHANA NA KOCHA WAO

SHIRIKISHO la kandanda la Ujerumani (DFB), limeweka bayana azma yake ya kuendelea na kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Joachim Loew.

Hatua hiyo imefuatia taarifa kuwa Shirikisho hilo lilikuwa mbioni kuachana na kocha huyo, hasa baada ya kushindwa kuipa taji la michuano ya Euro ya mwaka 2016 iliyofanyika Ufaransa.

Lakini DFB imekanusha vikali uvumi huo na kusisitiza kuwa wataendelea kuwa na mwalimu huyo, hasa katika kipindi hiki cha kujiandaa na mashindano ya fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.

Rais wa DFB, Reinhard Grindel ndiye alioyethibitisha hayo akivitaarifu vyombo vya habari nchini Ujerumani.


“Kwa heshima ya kocha wetu bingwa wa Dunia jogi anapaswa kuamua binafsi. Iwapo anataka kufanya uamuzi mara tu baada ya fainali za Kombe la Dunia, nitasema tufanye hivyo,” alisema Grindel. 

No comments