UMOJA WA "MDOMONI" WA VIONGOZI WA SIMBA WAMLIZA HASSAN DALALI

MWENYEKITI wa zamani wa zamani wa Simba, Hasani Dalali amelezea kusikitishwa na kitendo cha uongozi wa klabu hiyo kutomjali.

Dalali aliiambia Saluti5 kuwa licha ya yeye kufanya kazi kubwa ya kuleta umoja na mshikamano ndani ya Simba mwanzoni mwa msimu huu, lakini uongozi haumthamini.

Akasema hilo linatokana na yeye kuugua na kukaa ndani kwa takribani mwezi mmoja lakini hakuna kiongozi hata mmoja aliyediriki kwenda kumjulia hali.

Alisema hilo linathibitisha kuwa umoja wao upo midomoni lakini siyo moyoni kwani yeye ni miungoni mwa watu wanaosaidia uongozi huo kwa kiasi kikubwa kupigania mafanikio ya Simba.

“Nimeumwa mimi kwa siku 30 niliporudi tu kutoka Songea tulikoenda, nimeumwa kwa mwezi mzima nilienda kutibiwa Muhimbili, viongozi wote niliwapa taarifa lakini hakuna hata mmoja aliyekuja kunipa pole na kujua maandeleo yangu, sasa hii haileti picha ya umoja,’’ alisema Dalali.


Alisema, ingawa hilo haliwezekani kurudisha nyuma juhudi zake za kuipigania Simba, lakini anaona hayo sio maadili ya klabu hiyo na inapunguza imani yake kwa uongozi huu.

No comments