UWANJA WA KLABU YA SHANGHAI SHENHUA CHINA WATEKETEA KWA MOTO

UWANJA wa klabu ya Ligi Kuu ya China ya Shanghai Shenhua, umeteketea kwa moto uliotokea jana asubuhi.

Shirika la habari la China (Xhinhua), lilisema kuwa moto huo ulikuwa haujaathiri majukwaa au uwanja wa kuchezea na uchunguzi unaendelea ili kujua sababu.

Moto huo mkubwa ulioambatana na mosho ulizagaa na kusambaa katika uwanja huo wenye uwezo wa kubeba jumla ya watu 33,000 na kusababisha uwezekano wa klabu hiyo kucheza katika viwanja vingine.


Klabu hiyo inayonolewa na meneja wa zamani wa Brighton, Gus Poyet, ilimsaini mshambuliaji wa zamani wa Manchester City, Carlos Tevez mwaka jana.

No comments