AUDIO: BAADA YA KUTOSWA TWANGA, KAPOSHOO AIBUKIA FM ACADEMIA …Kutambulishwa Mango leo usiku
Mpiga tumba machachari Kaposhoo aliyekuwa akiitumikia Twanga Pepeta, ametua FM Academia “Wazee wa Ngwasuma”.

Kaposhoo ameithibitishia Saluti5 kuwa sasa yeye ni msanii wa FM Academia na ataanza rasmi kibarua chake leo usiku ndani ya ukumbi wa Mango Garden.


Mpiga tumba huyo mwenye mashabiki wengi,  alitoswa na Twanga Pepeta takriban miezi miwili iliyopita,  lakini hatimaye mlango mwingine wa rizki umefunguka na sasa anaungana na Wazee wa Ngwasuma.  

Msikilize Kaposhoo hapo juu akizungumzia safari yake ya kwenda  FM Academia.

No comments