VIONGOZI WA MATAWI YANGA WAKUTANA KUSUKA MPANGO WA KUIMALIZA AZAM FC

VIONGOZI wa matawi ya Yanga jijini Dar es Salaam wakiongozwa na wenyeviti na makatibu wao walikuta makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani kwa ajili ya kuandaa mipango ya kuimaliza Azam.

Mmoja wa viongozi hao ambaye hakutaka jina lake kuwekwa hadharani aliithibitishia Saluti5 juu ya kikao kilichofanyika siku ya Jumapili saa nane mchana ikiwa kama sehemu ya mkakati wa kuhakikisha Yanga inaibuka na ushindi katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Azam.

“Kama ijulikanavyo, mechi yetu na Azam ni ngumu na watani zetu wapo upande wa Azam, hivyo tutacheza na timu mbili ndiyo maana tumelazimika kuitana na kuweka mikakati yetu ambayo tayari tumekabidhi mapendekezo yetu kwa uongozi wa juu,” kilisema chanzo hicho kutoka ndani.

“Tutafanya kila liwezalo kuhakikisha tunaondoka na point zote tatu katika mchezo dhidi ya Azam ili kuwakata maini Simba ambao wanategemea mechi hiyo iwe mteremko  kwao,” aliongeza kiongozi huyo wa tawi.


Wakati huo huo timu hiyo imeingia kambini kwaajili ya mchezo huo muhimu huku wachezaji wakitamka neno moja tu, "Lazima tuibuke na ushindi.”

No comments